Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 01 Oktoba, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha elimu ya sheria nchini.