Post Details

RATIBA YA USIKILIZAJI WA MASHAURI YA MAHAKAMA INAYOTEMBEA 'MOBILE COURT' MIKOANI DSM NA MWANZA

Published By:Mary C. Gwera

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

                                                                                                         

MAHAKAMA YA TANZANIA

 

TANGAZO LA MAHAKAMA INAYOTEMBEA

 • Katika kuboresha huduma zake, Mahakama ya Tanzania inakuletea huduma bora na maalumu ya Mahakama Inayotembea (Mobile Court Services),
 • Mahakama Inayotembea imeanzishwa kwa ajili ya kusogeza huduma za Kimahakama karibu na wananchi.
 • Ewe mwananchi usitaabike kwenda kutafuta huduma za mahakama mbali na makazi yako, Mahakama ya Tanzania inakuletea huduma zake mtaani kwako.
 • Ewe Baba, Mama au Kijana usisite kufungua shauri lako katika Mahakama Inayotembea. Unaweza kufungua mashauri yafuatayo:-
 • Mirathi
 • Ndoa
 • Madai
 • Jinai, au
 • Kukata rufaa kutoka mabaraza ya kata
 • Pia waweza kupata huduma nyingine zifuatazo:-
 • Fomu mbalimbali za kufungulia mashauri, kama vile mirathi, ndoa na madai,
 • Kufungua mashauri ya kwa njia ya mtandao (“electronic filing”) kwa ngazi zote za Mahakama,
 • Kupata taarifa za mashauri kwa ngazi zote za Mahakama,
 • Kupata elimu na ushauri kuhusu huduma mbalimbali za mahakama
 • Kupata vipeperushi mbalimbali vinavyotoa taratibu za ufunguzi wa mashauri ya aina mbalimbali.
 • Ewe mwanachi okoa muda wako pamoja na gharama kwa kufungua shauri katika Mahakama Inayotembea.
 • Huduma hii itatolewa kwa utaratibu ufuatao;
 • Gari la Mahakama Inayotembea litakuwa katika vituo maalumu kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 8:30 mchana. Ratiba ya uskilizaji wa mashauri itakuwa kama ifuatavyo:-

 

       DAR ES SALAAM

SIKU

MUDA

KITUO

ENEO HUSIKA

WILAYA

JUMATATU

3:00-8:30

Bunju

Katika viunga vya Ofisi za Kata Bunju

Kinondoni

JUMANNE

3:00-8:30

Kibamba

Katika viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kibamba

Ubungo

JUMATANO

3:00-8:30

Buza

Kituo cha Dalala Buza

Temeke

ALHAMIS

3:00-8:30

Chanika

Eneo la Wazi karibu na Kituo cha Polisi Chanika

Ilala

IJUMAA

3:00-8:30

Kutoa Elimu kwa Umma katika maeneo mtakayotangaziwa.  

 

MWANZA

SIKU

MUDA

KITUO

ENEO HUSIKA

WILAYA

JUMATATU

3:00-8:30

Buswelu

Buswelu Sokoni

Ilemela

JUMANNE

3:00-8:30

Igoma

Eneo la Kupaki Malori

Nyamagana

JUMATANO

3:00-8:30

Igoma

Eneo la Kupaki Malori

Nyamagana

ALHAMIS

3:00-8:30

Buhongwa

Eneo la Wazi karibu na Kituo cha Polisi Buhongwa

Nyamagana

IJUMAA

3:00-8:30

Buhongwa

Eneo la Wazi karibu na Kituo cha Polisi Buhongwa

Nyamagana

 

 • Mashauri yatasikilizwa na kutolewa uamuzi ndani ya siku 1 mpaka 30.
 • Nakala ya hukumu itatolewa siku uamuzi ulipotolewa. 

 

Kumbuka: Mahakama Inayotembea itasikiliza mashauri ya madai yenye thamani isiyozidi Shillingi Millioni 30 na haitasikiliza wala kutoa maamuzi kwa mashauri yanayotokana na migogoro ya ardhi.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:-

Msajili Mkuu,

Mahakama ya Tanzania,

26 Barabara ya Kivukoni,

S.L.P. 9004

11409DAR ES SALAAM

TANZANIA

Telex:41838 CR TZ

Simu: 2124312

Fax:255-22-27724/

       255-22-2127656

Email:info.@judiciairy.go.tz

Tovuti:www.judiciary.go.tz  AU Mahakama yoyote iliyo karibu nawe.

 

Ukisikia tangazo hili tafadhari mjulishe aliyekaribu nawe.

 

Kwa pamoja tunaboresha huduma: usisite kutoa maoni”

 

Tangazo hili limetolewa na Uongozi wa Mahakama

 

Comments (1)

 • Photo Loading... Michael Aristid

  Tunashukuru sana tunaomba nasi Kilimanjaro tupate mobile court wengine hawawezi kufikia mahakama kutokana na umbali

  27-08-2019

Leave a Comment