Post Details

WASAIDIZI WAPYA WA SHERIA WA MAJAJI WAPATIWA ‘ABC’ ZA UTENDAJI KAZI

Published By:Mary C. Gwera

Jumla ya Wasaidizi wa Sheria 21 wa  Majaji wa Mahakama  ya Rufani (T) walioteuliwa hivi karibuni wamepatiwa utangulizi wa masuala muhimu ya kuzingatia katika ufanyaji kazi kwenye Mahakama hiyo.

Akizungumza na Maafisa hao mapema Agosti 15, 2019 katika Ukumbi ya Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati amewaasa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mahakama imewaamini, hivyo basi ni vyema mkafanye kazi kwa uadilifu na unyenyekevu,” alieleza Msajili Mkuu.

Mbali na masuala hayo, Mhe. Revocati aliongeza kwa kuwataka Maafisa hao kutojihusisha na vitendo vya upokeaji wa rushwa wanapotekeleza majukumu yao.

“Siku hizi hakuna rushwa isiyojulikana pindi unapojihusisha katika vitendo hivi utajulikana tu, hivyo ni vyema kutojihusisha ili kuwa salama,” alisisitiza Mhe. Revocati.

Wasaidizi hao wa Sheria ambao kwa taaluma ni Mahakimu wameteuliwa kutoka Mahakama mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuwasaidia Waheshimiwa Majaji katika kufanya tafiti ambazo zitawawezesha katika utoaji wa maamuzi ya rufaa mbalimbali.

Kabla ya kuanza kazi rasmi Maafisa hao watapatiwa Mafunzo elekezi yatakayowawezesha kuwapa kwa kina misingi ya ufanyaji kazi katika Mahakama hiyo

Comments (1)

  • Photo Loading... Elisha mosses

    Jambo jema lakin pia mahakimu katika mahakama za ngazi za chini hawatoshelezi tunaiomba serikali lakni pia tume ya utumishi wa mahakama kuliangalia Hilo na kulitafutia ufumbuzi ilikurahisisha utoaji wa haki kwa wakati asanteh

    16-08-2019

Leave a Comment