Post Details

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, MHE.PROJEST RUGAZIA AFARIKI DUNIA

Published By:Mary C. Gwera

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Projestus Aloyce Rugazia (pichani) amefariki dunia.

Mhe. Jaji Rugazia amefariki dunia alfajiri ya kuamkia Agosti 04, 2019 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa-Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Msiba upo nyumbani kwake Kinondoni- Dar es Salaam, ratiba ya taratibu za kuaga na mazishi itajulikana mapema Agosti 05, 2019.

Marehemu Jaji Rugazia alizaliwa Agosti 28, 1954 mkoani Kagera, alianza kazi rasmi Januari 01, 1983 kama Hakimu Mkazi.

Marehemu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Machi 28, 2003. Aidha; Marehemu Jaji Rugazia alistaafu rasmi Agosti 28, 2016 akitokea Mahakama Kuu-Divisheni ya Ardhi.

Mahakama ya Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

 

IMETOLEWA NA:-  KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,

                               MAHAKAMA YA TANZANIA.

Comments (1)

  • Photo Loading... magesa.masige

    Mungu aitie nguvu familia yake ktk kipindi hiki kidumu

    08-08-2019

Leave a Comment