Post Details

WAJUMBE WA MENEJIMENTI YA MAHAKAMA YA TANZANIA WAKAGUA JENGO JIPYA LA MAHAKAMA KUU-KANDA YA MUSOMA

Published By:Mary C. Gwera

 Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania wametembelea jengo jipya la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kwa lengo la kulikagua kufuatia kukamilika kwake kwa asilimia kubwa. Ukaguzi huo ulifanyika Julai 12, 2019.

Upatikanaji wa huduma ya Mahakama Kuu mkoani Mara utawarahisishia wananchi wa mkoa huu kuondokana na aza ya kusafiri kufuata huduma ya Mahakama Kuu- Kanda ya Mwanza umbali wa zaidi ya kilomita 200.

Katika ziara hiyo, Wajumbe hao wametembelea Ofisi ya muda ya Jaji Mfawidhi- Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma, wamekagua pia ujenzi wa nyumba mbili za  Majaji wa Kanda hiyo.

Comments (1)

  • Photo Loading... JAMILA JAMALI

    MAHAKAMA MKO JUU JENGO NZURI SANA

    11-09-2019

Leave a Comment