Post Details

MAWAKILI WAPYA 720 WAAPISHWA NA JAJI MKUU WA TANZANIA

Published By:Mary C. Gwera

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewakubali na kuwapokea jumla ya Mawakili wapya 720 katika Sherehe ya 60 iliyofanyika mapema Julai 19, 2019 katika Viwanja vya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania 'Law School of Tanzania'.

Miongoni mwa waliopata Uwakili katika sherehe hizi ni pamoja na baadhi ya Maafisa wa Mahakama ya Tanzania wakiwemo, Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu, Manaibu Wasajili na Mahakimu.

Comments (0)

Leave a Comment