Post Details

UTEUZI; JAJI MWAMBEGELE ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA NEC

Published By:Mary C. Gwera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji Jacob Mwambegele kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa tarehe 27 Desemba, 2021 na Mkurugenzi  wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Jaffar Haniu inasema Jaji Mwambegele ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Semistocles Kaijage ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huohu, Mhe. Rais Samia amemteua Jaji Mwanaisha Kwariko kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Jaji Kwariko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Jacob Mwambegele ambaye ametueliwa kuwa Mwenyekiti wa (NEC).

Aidha, katika taarifa hiyo, Rais Samia amemteua pia Jaji Sam Rumanyika, Jaji wa Mahakama Kuu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani (T).

Comments (0)

Leave a Comment