Post Details

JAJI MWAIKUGILE AZIKWA

Published By:Mary C. Gwera

Na Margreth Kinabo, Mahakama.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma jana tarehe 24 Novemba, 2021 ameongoza mamia ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wananchi wengine kuuaga mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Njengafibili Mwaikugile aliyefariki dunia tarehe 20 Novemba, 2021 jijini Dar es Salaam.

Shughuli za kuaga mwili wa marehemu Mwaikugile zilifanyika nyumbani kwake Sala Sala Juu Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wa Mahakama na Majaji wastaafu walishiriki. Viongozi wengine wa Mahakama waliohudhuria maziko hayo ni Jaji Kiongozi, Mhe. Mustapher Siyani, Msajili Mkuu, Mhe. Wilbert Chuma, Mtendaji Mkuu, Prof. Elisante Ole Gabriel na baadhi ya Majaji wastaafu, akiwemo Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta.

Baada ya heshima za mwisho kutolewa nyumbani kwake, mwili wa marahemu ulipelekwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa ajili ya ibada kabla ya kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Marehemu Mwaikugile alianza kuhudumu katika Mahakama ya Tanzania tangu 1982 kama Hakimu na baadaye kupanda katika ngazi mbalimbali za utumishi kama Msajili wa Mahakama Kuu na baadaye Mahakama ya Rufani kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu tarehe 28 Februari, 2003, nafasi ambayo ameitumikia hadi alipostaafu tarehe 15 Oktoba, 20214.

Comments (0)

Leave a Comment