Post Details

JAJI MAKARAMBA ASTAAFU RASMI- AWASHUKURU VIONGOZI NA WATUMISHI WA MAHAKAMA KWA USHIRIKIANO

Published By:Mary C. Gwera

Aliyekuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert V. Makaramba amestaafu rasmi baada ya kufikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi kati yake na Jaji Mfawidhi mpya wa Kanda hiyo, Mhe. Dkt. John Utamwa Aprili 30, 2019, Mhe. Jaji Mstaafu Makaramba  aliwashukuru viongozi na watumishi wote wa Kanda ya Mbeya kwa ushirikiano na upendo mkubwa waliompatia tangu alipowasili katika Kanda hiyo na kuwaomba kuhamishia nguvu hiyo kwa Jaji Mfawidhi mpya.

Naye Jaji Mfawidhi mpya, Mhe. Dkt. Utamwa aliwataka viongozi na watumishi wote kumpa ushirikiano kwa kuwa kila mtumishi ana mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku. 

“Ili kuifikia Dira ya Mahakama isemayo Haki Sawa kwa Wote na kwa Wakati  kila mtumishi ana nafasi yake bila kujali cheo au wadhifa alionao,” alisisitiza Mhe. Jaji Utamwa.

Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na Wahe. Majaji waliohamishimiwa katika Kanda hiyo ambao ni Mhe. Dkt. Adam J. Mambi, Mhe. Dunstan B. Ndunguru na Mhe. Dkt. Lilian M. Mongella. 

Comments (2)

  • Photo Loading... Marco MMS Mabala

    Makutakia mapumziko mema Jaji wangu mwadilifu, uliyeipenda kazi yako, ulitoa maamuzi kwa weledi, bila upendeleo na ulikuwa msaada mkubwa sana kwa watumishi wote. Tutakosa miongozo yako. Naomba uendelee kuwafundisha Mawakili na hasa kuhusu mambo ya Arbitration. Namuomba Jaji wetu Mkuu asikuache hivi hivi ni vyema update kazi nyingine ya kuwatumikia Watanzania kwani bado una nguvu za kutosha.

    14-05-2019
  • Photo Loading... Baraka Mbwilo

    Tunakutakia Maisha mema na marefu ili tuzidi kufaidi weledi wako ktk tasnia ya sharia. Tunakukaribisha kwenye uwakili na katika kipindi hiki ambacho mawakili vijana ni wengi usichoke kutufundisha, kuonya na kutoa mwelekeo sahihi tunaotakiwa vijana tuufuate kwenye hii taaluma. Mungu akubariki.

    19-05-2019

Leave a Comment