Post Details

RAIS SAMIA ATUMA SALAAM ZA POLE KWA JAJI MKUU

Published By:LYDIA CHURI

Na Lydia Churi-Mahakama

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtumia salaam za rambirambi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Njengafibili Mponjoli Mwaikugile kilichotokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bw. Jaffar Haniu tarehe 20 Novemba, 2021 jijini Dar es salaam, Rais Samia amesikitiswa na kifo cha Jaji Mstaafu Mwaikugile kwa kuwa alikuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa.

Katika taarifa hiyo, Rais ametoa pole kwa Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na wanafamilia wote wa Mahakama na kuw omba kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi na pia amemuombea marehemu apumzike mahali pema peponi.

Kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt, Jaji Mwaikugile alikutwa na umauti tarehe 20 Novemba, 2021 jijini Dar es Salaam.

Taratibu za mazishi zinaendelea, ambapo; taarifa za awali zinasema kuwa marehemu Jaji Mwaikugile atazikwa siku ya Jumatano tarehe 24 Novemba, 2021 jijini Dar es Salaam. Msiba upo nyumbani kwake Salasala, Dar es Salaam.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

 

Comments (0)

Leave a Comment