Post Details

TANZIA; JAJI MSTAAFU MWAIKUGILE AFARIKI DUNIA

Published By:Mary C. Gwera

TANZIA

Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Njengafibili M. Mwaikugile (katika picha juu).

Kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt, Jaji Mwaikugile alikutwa na umauti alfajiri ya kuamkia leo tarehe 20 Novemba, 2021 jijini Dar es Salaam.

Taratibu za mazishi zinaendelea, ambapo; taarifa za awali zinasema kuwa marehemu Jaji Mwaikugile atapumzishwa katika makazi yake ya milele siku ya Jumatano tarehe 24 Novemba, 2021 jijini Dar es Salaam. Msiba upo nyumbani kwake Salasala-Dar es Salaam.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 

Comments (0)

Leave a Comment