Post Details

MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA AKAGUA UKARABATI WA JENGO LA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MOSHI

Published By:LYDIA CHURI

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel alifanya ziara ya kikazi Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya watumishi wa kanda hiyo.

Prof. Ole Gabriel amewataka watumishi wa kanda hiyo kuzingatia mambo matano muhimu wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. 

Aliyataja mambo hayo kuwa ni kutobaguana kwa namna yoyote, kutojihusisha na vitendo vya rushwa, uvivu na uzembe na kutochelewesha mashauri mahakamani pasipokuwa na sababu za msingi.

Aidha, Mtendaji Mkuu wa Mahakama alitembelea na kukagua kazi ya ukarabati wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi. 

Comments (0)

Leave a Comment