Post Details

JAJI KIONGOZI AWASILI MKOANI MBEYA KWA ZIARA YA KIKAZI

Published By:Mary C. Gwera

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi amewasili Mkoani Mbeya Aprili 08, 2019 kuanza rasmi ziara ya kikazi katika Kanda hiyo ya Mahakama.

Katika ziara yake ya siku mbili (2) ndani ya Kanda hiyo, Mhe. Jaji Kiongozi, anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa Mahakama inayoendelea pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Mahakama katika Kanda hiyo.

Lengo la ziara ni kujua  hali ya maendeleo ya utekelezaji wa maboresho ya huduma mbalimbali za  Mahakama na vilevile kuwakumbusha Watumishi wa Mhimili huu kuendelea kutekeleza jukumu la msingi la utoaji haki nchini kwa ubora wa hali ya juu kwa manufaa ya wananchi.

Comments (0)

Leave a Comment