Post Details

JAJI MSTAAFU RAYMOND RUHUMBIKA AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Raymond Juma Louis Ruhumbika amefariki dunia jana Agosti 23, 2021 katika hospitali ya mkoa wa Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Mahakama, taarifa zaidi kuhusiana na msiba wa Jaji Mstaafu Ruhumbika zitapatikana hapo baadaye.

Marehemu Jaji Ruhumbika alizaliwa Machi 17 mwaka 1933 mkoani Mwanza. Aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania April 1, mwaka 1964. Aidha, Juni 29 mwaka 1981 aliteuliwa na Rais wa awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Alikitumikia cheo hicho mpaka Machi 17 mwaka 1993 alipostaafu kwa mujibu wa sheria.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki pamoja na watumishi wote wa Mahakama kufuatia msiba huo.

 

                                              BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE

 

 

Comments (0)

Leave a Comment