Post Details

JENGO LA MAHAKAMA YA MWANZO HAYDOM MANYARA MBIONI KUKAMILIKA

Published By:Mary C. Gwera

Ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Haydom, Wilayani Mbulu Mkoani Manyara uko mbioni kukamilika.

Hayo yamebainika na Uongozi wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara kufuatia ziara ya ki kukagua mradi wa jengo hilo iliyofanyika hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa jengo hilo linatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 09, mwaka huu.


Katika kikao ‘site meeting’ iliyofanyika mara baada ya ukaguzi kilichohudhuriwa na Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Manyara Bwana Jacob Swalle, Meneja wa TBA Mkoa wa Manyara Bwana  Wilson Tesha na Mwakilishi wa kamupuni ya ECO GREEN Construction Co Ltd (ambaye ni Mkandarasi wa Jengo hilo) Bwana Noah Haki, ilibainika kuwa jengo hilo limekamilika kwa kiasi cha asilimia 65.

Mradi wa Ujenzi wa jengo hilo ulianza tarehe 03/03/2021. Mahakama ya Mwanzo Haydom inatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambao kwa muda mrefu sasa  wamekuwa wakisafiri kwenda Dongobesh kwa ajili ya huduma za kimahakama ambapo kuna umbali wa Kilomita 45.

Comments (0)

Leave a Comment