Post Details

TANZIA; HAKIMU MKAZI MFAWIDHI WA MAHAKAMA YA WILAYA SERENGETI AFARIKI DUNIA

Published By:Mary C. Gwera

TANZIA

Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti-Mara, Mhe. Ismael Emmanuel Ngaile (pichani) kilichotokea siku ya Jumatano Agosti 11, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na Uongozi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma marehemu Ngaile alikuwa na umauti katika hospitali ya Nyerere DHH iliyoko wilayani Serengeti alipokuwa akipatiwa matibabu.

Marehemu Ngaile aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania Juni 27, 2006, na alifanya kazi katika vituo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Wilaya Kibondo..

Taratibu za mazishi zinaendelea, aidha; taarifa za awali zinasema kuwa marehemu atapumzishwa nyumbani kwake wilayani Kahama.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments (0)

Leave a Comment