Post Details

TANZIA; HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO BUGURUNI AFARIKI DUNIA

Published By:Mary C. Gwera

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Mhe. Mwinyiheri Mohamed Kondo (pichani) aliyekuwa Hakimu katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala zinasema kuwa marehemu Kondo alikutwa na umauti alfajiri ya kuamkia jana Julai 22, 2021 nyumbani kwake Toangoma Mikwambe jijini Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa leo Julai 23, 2021 nyumbani kwake Toangoma-Mikwambe jijini Dar es Salaam.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments (0)

Leave a Comment