Post Details

MAWAKILI SASA KUAPA KIAPO CHA UADILIFU

Published By:LYDIA CHURI

Na Lydia Churi- Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameridhia ombi la Chama cha Mawakili Tanganyika (Tanganyika Law Society-TLS) la wanasheria wanaokubaliwa na kupokelewa kuwa mawakili kuongezewa kiapo cha uadilifu.

Ombi hilo lilitolewa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania jana na Z “Kiapo cha uadilifu ni utaratibu unaotumika hata kwa viongozi wengine wanapoapishwa hivyo mimi sina pingamizi, kuna haja ya kukumbushana umuhimu wa maadili kwenye kazi za utoaji haki”, alisema Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu alisema Chama cha Mawakili Tanganyika ni wadau muhimu kwenye utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania kwa kuwa mafanikio ya mhimili huo yanatokana na mchango mkubwa unaotolewa na chama hicho.

Kwa Upande wake, Rais wa TLS ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa matumizi ya Tehama pamoja na kutoa miongozo mbalimbali inayorahisisha upatikanaji wa haki nchini.

Alisema miongozo inayotolewa na Mahakama imesaidia kurahisisha upatikanaji wa haki huku akitolea mfano wa mwongozo kutoa adhabu (sentencing Manual) pamoja na ule wa masuala ya dhamana.

“Chama cha Mawakili Tanganyika kitaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati yake na Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kuboresha shughuli za utoaji haki nchini na kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati”, alisema.

Kuhusu changamoto za chama hicho, Prof. Hosea alisema hivi sasa baadhi ya Taasisi zikiwemo za Serikali zimekuwa zikikataa viapo vya mawakili na kuelekeza matumizi ya viapo vinavyotoka mahakamani. Aidha, alimwomba Jaji Mkuu kukisaidia chama hicho ili viapo vya wananchama wake vikubalike kwa wote kama ambavyo sheria imeruhusu.

 

 

 

 

Comments (0)

Leave a Comment