Post Details

MAHAKAMA YA TANZANIA YAENDELEA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA 'SABASABA'

Published By:Mary C. Gwera

Wananchi mbalimbali wanaotembelea katika banda la Mahakama ya Tanzania linaloshiriki katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba' 2021 wanaendelea kupata huduma. Pichani ni baadhi ya matukio katika picha yakionyesha wananchi mbalimbali wakipata huduma za kimahakama pamoja na huduma za Wadau wa Mahakama wanaoshiriki pamoja na Mahakama katika Maonesho hayo.

Huduma zinazotolewa ni pamoja na Usikilizwaji wa mashauri katika Mahakama inayotembea 'mobile court', Maboresho ya Mahakama, Mahakama mtandao, kuelezea taratibu za Mirathi na Wosia, elimu ya Mahakama ya Ardhi, Biashara, Kazi na Kitengo cha Usuluhishi 'mediation' na kadhalika.

Comments (0)

Leave a Comment