Post Details

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA HUDUMA KATIKA BANDA LA MAHAKAMA 'SABASABA'

Published By:Mary C. Gwera

Mahakama ya Tanzania inaendelea kushiriki katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba', 2021                                                                                      

  MAHAKAMA YA TANZANIA INAPENDA KUWAJULISHA WANANCHI NA WADAU WOTE KWA UJUMLA KUWA INASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 45 YA BIASHARA YA KIMATAIFA ‘SABASABA’ YALIYOANZA RASMI JUMATATU JUNI 28, 2021.

KATIKA KIPINDI CHA MAONESHO HAYO, MAHAKAMA INAKUSUDIA KUTOA HUDUMA ZIFUATAZO: -

1. HUDUMA YA MAHAKAMA INAYOTEMBEA ‘MOBILE COURT SERVICES’

2. KUSIKILIZA BAADHI YA MASHAURI KWA NJIA YA MTANDAO KWA KUTUMIA MAHAKAMA MTANDAO ‘VIRTUAL COURT’

3. ELIMU JUU YA HUDUMA NA TARATIBU MBALIMBALI ZA UFUNGUAJI WA MASHAURI YAKIWEMO MASHAURI YA MIRATHI.

4. KUELEZEA MFUMO WA KUSAJILI, KURATIBU NA KUSIMAMIA UENDESHAJI WA MASHAURI (JSDS)

5. KUTOA MAELEKEZO YA UPATIKANAJI WA MAAMUZI KWA NJIA YA MTANDAO

6. KUELEZA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA NGAZI MBALIMBALI ZA MAHAKAMA IKIWEMO DIVISHENI ZA MAHAKAMA KUU

7. KUSIKILIZA NA KUTOLEA SULUHU MALALAMIKO YA WANANCHI

8. KUTOA FOMU ZA UDAHILI NA KUZIPOKEA AMBAPO HUDUMA HII ITATOLEWA NA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA (IJA)

9. MSAADA WA KISHERIA ‘TLS’

AIDHA; KATIKA MAONESHO HAYO MAHAKAMA YA TANZANIA ITAKUWA KATIKA BANDA MOJA PAMOJA NA BAADHI YA WADAU WAKE AMBAO NI CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA-LUSHOTO, (IJA), CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS), CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA) PAMOJA NA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI (EACJ), AMBAO WOTE WATATOA ELIMU KUHUSU MAENEO YAO.

HUDUMA TAJWA ZITAKUWA ZIKITOLEWA NDANI YA BANDA LA MAHAKAMA, LILILOPO MKABALA NA BANDA LA JKT KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE ‘SABASABA’ DAR ES SALAAM.

HUDUMA HIZO ZITATOLEWA HADI JULAI 08, 2021.

EWE MWANANCHI, KARIBU UPATE ELIMU YA SHERIA PAMOJA NA KUTOA MAONI YAKO ILI KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.

WOTE MNAKARIBISHWA.

 

Comments (0)

Leave a Comment