Post Details

MAHAKIMU KANDA YA MUSOMA WANOLEWA KWA KAZI

Published By:Mary C. Gwera

Mahakimu Wakazi Kanda ya Musoma wanolewa kikamilifu katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mhe. Jaji. Mfawidhi wa Kanda ya Musoma Mhe. Jaji, John Kahyoza ambapo, Mahakimu hao walikumbushwa kuzingatia maadili ya kazi pamoja na taratibu mbalimbali katika usikilizaji wa Mashauri mbalimbali.

Katika kikao kazi hicho kilichofanyika hivi karibuni, Mahakimu hao walipewa jukumu la kuandaa na kuwasilisha mada tofauti tofauti na kisha kufanyika majadiliano ya pamoja.

Mada zilizowasilishwa ni pamoja na Tabia na mwenendo wa Maadili kwa Maafisa wa Mahakama, Hatua muhimu za kuzingatia katika uendeshaji wa Mashahuri ya Jinai tangu kufunguliwa hadi kufikia hukumu, Ufunguaji wa kesi katika Mahakama za Mwanzo.

Nyingine ni hatua za utekelezaji wa hukumu katika Mahakama za Mwanzo, Jinsi ya kushughulikia mapingamizi katika mashauri ya mirathi Mahakama za Mwanzo na Uendeshaji wa Mashauri ya Jinai katika Mahakama za Mwanzo.

Washiriki wa kikao kazi hicho walimpongeza Mhe. Jaji. Kahyoza kwa kuandaa kikao hicho kwani kimesaidia kuwakumbusha mambo muhimu ya kuzingatia katika utendaji kazi wa kila siku na pia kimekuwa msaada kwa Mahakimu ambao ndio wameanza kazi.

 

Comments (0)

Leave a Comment