Post Details

JAJI KIONGOZI AWASILI MKOANI IRINGA KUANZA ZIARA YA KIKAZI KATIKA KANDA HIYO NA MBEYA

Published By:Mary C. Gwera

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi mapema leo Aprili 04, 2019 amewasili Mkoani Iringa kuanza rasmi ziara ya kikazi katika Mahakama Kanda ya Iringa pamoja na Kanda ya Mbeya.

Katika ziara yake Mhe. Jaji Kiongozi, anatarajiwa kuongoza hafla ya kumuaga rasmi kitaaluma, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa, Mhe. Jaji Mary Shangali itakayofanyika Aprili 05, 2019 katika Ukumbi ya Mahakama Kuu-Iringa.

Aidha Mhe. Jaji Dkt. Feleshi atapata wasaa wa kuongea na Watumishi pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa Mahakama inayoendelea katika Kanda hizo mbili.

Lengo la ziara ni kujua  hali ya maendeleo ya utekelezaji wa maboresho ya huduma mbalimbali za  Mahakama na vilevile kuwakumbusha Watumishi wa Mhimili huu kuendelea kutekeleza jukumu la msingi la utoaji haki nchini kwa ubora wa hali ya juu kwa manufaa ya wananchi ambao ndio walengwa wakuu.

Baada ya kukamilisha ziara yake Kanda ya Iringa, Mhe. Jaji  Kiongozi, atafanya ziara pia Kanda ya Mbeya.

Comments (0)

Leave a Comment