Post Details

HAKIMU MAHAKAMA YA MWANZO MASUMBWE MKOANI GEITA AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

                                                                                              TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Masumbwe wilayani Bukombe Mhe. Joyce Kalokola kilichotekea usiku wa kuamkia leo tarehe 29/05/2021 nyumbani kwako jijini Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza inasema marehemu Kalokola alipata ya ajali ya bus iliyotokea Mei 9, 2021 katika Kijiji cha Tumuli mkoani Singida alipokuwa akirejea kituoni kwake.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Marehemu alilazwa hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma kwa ajili ya matibabu baada ya kuumia uti wa mgongo, alitibiwa na baadaye kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya yake kuimarika.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Maduka Manne jijini Dar es salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne Juni 1, 2021 jijini Dar es salaam. Taratibu nyingine za mazishi zitajulikana baadaye.

Mahakama inawapa pole ndugu, jamaa, marafiki na watumishi wote wa Mahakama ya Tanzania.

  BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments (0)

Leave a Comment