Post Details

KUNDI LA PILI LA NAIBU WASAJILI NA WATENDAJI WAANZA MAFUNZO YA UTUNZAJI KUMBUKUMBU

Published By:Mary C. Gwera

Matukio katika picha, hafla ya ufunguzi rasmi wa Mafunzo elekezi ya Utunzaji Kumbukumbu na Nyaraka za Mahakama kwa kundi la pili la Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dar es Salaam.

Akifungua mafunzo hayo Aprili 14, 2021, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu-Kanda ya Dodoma, Mhe. Mustapher Siyani amewasisitiza Washiriki hao kuendelea kushiriki ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuboresha huduma za Mahakama kwa manufaa ya wananchi.

Katika mafunzo hayo ya siku tatu (3) yaliyoanza rasmi leo Aprili 15, 2021 hadi Aprili 17, 2021 Washiriki watapitishwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya majalada na uandishi wa nyaraka mbalimbali, usajili wa mashauri kwa mfumo wa kielektroniki, usimamizi na ukaguzi wa Mahakama, usimamizi wa masuala ya fedha na kumbukumbu zake kupitia mfumo mpya wa ‘MUSE’ na mifumo ya ndani na usimamizi wa bajeti.

Comments (0)

Leave a Comment