Post Details

MTUMISHI WA MAHAKAMA AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

                                                 

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bi. Rehema Machunda aliyekuwa Msaidizi wa Kumbukumbu Mwandamizi katika Masjala ya Wazi Mahakama ya Rufani.

Mtumishi huyo alifariki dunia jana Tarehe 14/4/2021 katika hospitali ya Temeke alipokuwa akipatiwa matibabu.

Msiba uko nyumbani kwake Mbagala-Saku Mwisho. Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehre 17/4/2021 huko Mbagala, jijini Dar es salaam.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.  

Comments (0)

Leave a Comment