Post Details

TANZIA; HAKIMU MKAZI MFAWIDHI MBARALI AFARIKI DUNIA

Published By:Mary C. Gwera

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mbarali-Mbeya, Mhe. Agripina Wokusima Kimaze (pichani).

Taarifa zinasema kuwa marehemu Agripina alifikwa na umauti alfajiri ya kuamkia Aprili 07, 2021 mkoani Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Aidha, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya-Kisarawe.

Mwili utasafirishwa kwa ndege Aprili 09, 2021 kuelekea Kagera-Bukoba kwa ajili ya maziko

Tarehe ya maziko itapangwa na ndugu wa marehemu na marehemu anatarajiwa kuzikwa eneo la Buhembe jirani na Shule ya Sekondari ya Ihungo Bukoba mjini.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu mzito wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments (0)

Leave a Comment