Post Details

BURIANI RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Published By:LYDIA CHURI

                                                                JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

                                                                                      MAHAKAMA

                                                                      

JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA, MENEJIMENTI NA WATUMISHI WOTE WA MAHAKAMA WANAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA ULIOTUPATA KUFUATIA KIFO CHA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.

MAHAKAMA YA TANZANIA INATOA SALAAM ZA POLE KWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN PAMOJA NA VIONGOZI WOTE WA SERIKALI.

RAIS MAGUFULI ATAKUMBUKWA KWA MCHANGO WAKE ALIOUTOA KWA MAHAKAMA IKIWEMO KUIMARISHA MIUNDO MBINU YA MAHAKAMA NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KWA KUWEZESHA UANZISHWAJI WA DIVISHENI YA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI YA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA.

                                             BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE

Comments (0)

Leave a Comment