Post Details

TANZIA, MTUMISHI WA MAHAKAMA AFARIKI DUNIA

Published By:Mary C. Gwera

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bw. Athuman Juma (pichani) kilichotokea jana usiku Machi 15, 2021 katika hospitali ya Amana-Dar es Salaam.

Marehemu Juma alikuwa Dereva wa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Msajili Mkuu inasema mazishi yanatarajia kufanyika leo Machi 16, 2021 Kibaha-Pwani.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu mzito wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments (0)

Leave a Comment