Published By: | Mary C. Gwera |
---|
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Mhe. Bridget Mathew Sengwaji aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Wilaya Mkuranga kwa nafasi ya Hakimu Mkazi.
Kwa mujibu wa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha-Pwani, Mhe. Joyce Mkhoi, marehemu Bridget alikutwa na umauti tarehe 27 Oktoba, 2024 katika hospitali ya Haemada iliyopo Mabwepande Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla.
Mhe. Mkhoi amesema kuwa mazishi yatafanyika leo tarehe 29 Oktoba, 2024 katika makaburi ya Kondo Ununio jijini Dar es Salaam.
Marehemu Bridget Mathew Sengwaji aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania mwaka 2012 kama Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Mwanzo Manundu Wilaya ya Korogwe na kuhudumu mpaka mwaka 2019. Aidha, mwaka 2019 alihamishiwa Mahakama ya Rufani Tanzania kama Msaidizi wa Sheria wa Jaji hadi Machi, 2024, mwezi Aprili, 2024 marehemu alihamishiwa Mahakama ya Wilaya Mkuranga ambapo alihudumu mpaka mauti yalipomfika.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.