Post Details

MTUMISHI WA MAHAKAMA YA MWANZO UKONGA AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bibi Salima Mohamed aliyekuwa Mtunza kumbukumbu wa Mahakama ya Mwanzo Ukonga kilichotokea jana tarehe 3//3/2021 nyumbani kwake Ukonga jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Aidha, kufuatia kifo hicho, mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao wilayani Newala mkoani Mtwara kwa ajili ya maziko. yanayotarajiwa kufanyika kesho, Ijumaa tarehe 5/3/2021.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

Comments (0)

Leave a Comment