Published By: | Mary C. Gwera |
---|
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bw. Jackson Lutengano Msokwa (katika picha) aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Mwanzo Uyole Mbeya kwa Cheo cha Msaidizi wa Kumbukumbu
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya, Bi. Mavis Miti msiba umetokea usiku wa tarehe 03 Agosti 2024 kwa ajali ya kugongwa na Gari akiwa njiani kwenye pikipiki yake akielekea nyumbani kwake Mswiswi Wilaya ya Mbarali.
Bi. Mavis amesema mazishi yatafanyika tarehe 6 August 2024 katika kijiji cha Itende Kati.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba wa mpendwa wetu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.