Post Details

TUME YA KUANDAA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 YAMTEMBELEA MSAJILI MKUU

Published By:innocent.kansha

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya ametoa rai kwa Viongozi wa Tume ya Taifa ya kuandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kuweka misingi bora ya kuimarisha utawala bora na utawala wa sheria, kwa kuweka bayana misingi ya Demokrasia, uhuru wa kujieleza na haki za binadamu ili iweze kujikita zaidi katika kuhimiza kulinda haki za binadamu.

Akizungumza na Ujumbe wa Tume hiyo uliyomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana tarehe 18 Juni, 2024, kwa lengo la kupata maoni yake kuhusu maeneo yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kuandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Mhe Nkya aliainisha kuwa wakati wa kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo itakayo ishishia mwaka 2050 inapaswa kuzingatia mambo mbalimbali yanayolenga ustawi wa Taifa, ikiwa ni pamoja na kulenge kuimiarisha ulinzi wa mazingira pamoja na namna bora ya kukabili na mabadiliko ya Tabia nchi.

’’Nitoe rai kwa Viongozi wa Tume ya Mipango ya kuona namna bora ya kupata na kupokea maoni ya Mhimili wa Mahakama kwa pamoja na siyo ya mtumishi mmoja mmoja,” alisistiza Msajili Mkuu.

Aidha, Mhe. Nkya aliongeza kuwa, Dira pia ilenge kuwa na Tanzania yenye Uchumi imara na Siasa safi (Economic, Social and Political Stability). Na pia, Dira ilenge kuimarisha Tanzania ya kidijitali kwa kusisistiza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Vilevile Dira ilenge kutengeneza mazingira ya namna bora ya kutumia maliasili zinazopatikana nchini kwa masilahi mapana ya nchi.

Vilevile, Mhe. Nkya alisema, Diara iangazie Mikakati mbalimbali ya namna ya kufikia maeneo ya kuwekeza zaidi kwenye rasilimali watu na kuwa na elimu bora zaidi, na pia kuwa na mikakati bora ya kutumia maliasili za nchi mfano, kuvua au kuvuna Samaki wanaopatikana kwenye kina kirefu cha bahari (deep sea) pamoja na namna ya kutumia rasilimali za asili kama vile madini, gesi asili kwa maendeleo ya Taifa.

Msajili Mkuu alihimiza Dira kuimarisha Sekta binafsi na kuwa na miundombinu inayowezesha kuyafikia masoko kwa urahisi. Kuhakikisha mipango ya Mahakama ya kuzogeza huduma ya utoaji wa haki kwa wananchi kwa wakati na kwa gharama nafuu inatekelezwa.

Comments (0)

Leave a Comment