Post Details

JAJI BARTHY :KUWENI MABALOZI WAZURI WA UKATILI WA KINGONO NA KIJINSIA

Published By:magreth.kinabo

Na Magreth Kinabo- Mahakama 

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Masuala ya Familia (IJC) Temeke, Mhe. Glady’s Nancy Barthy amewasihi mahakimu waliopatiwa mafunzo ya unyanyasaji wa kingono na ukatili wa jinsia wawe mabalozi wazuri elimu hiyo kwa wengine.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kituoni hapo kwa siku tatu yamefungwa  jana na Mhe. Barthy na yamehusisha mahakimu kutoka ngazi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambaye amewataka kuendelea kujifunza wenyewe elimu waliyopatiwa ili waweze kuwa wabobezi,kwa kuwa suala hilo ni endelevu.

“Ni utamaduni mzuri pale unapotoka kufanya mafunzo na wewe ukaenda kuwekeza na kuwafundisha wale ambao wako katika maeneo yetu ya kazi, kwa hiyo inafaa kuenda kuwafundisha wengine, na unapowafundisha wengine inakujengea uwezo na ujuzi zaidi, katika eneo ambalo unalitolea mafunzo.

“Ni muhimu kutambua ya kwamba jukumu la Jaji au Hakimu katika kuhakikisha anazingatia wadawa au mashahidi walio katika makundi ya maalum au yenye changamoto yanayohitaji kuangaliwa kwa upekee mfano wazee, watoto na walemavu na wale wote wanaohitaji msaada wa kipekee katika kuhakikisha kwamba haki inatendeka,”alisema Mhe Jaji Barthy. 

Aliongeza kuwa upande mashauri yanayohusu watoto ni muhimu kuzingatia Sheria ya Mtoto na kanuni zake.

Mhe. Jaji Barthy alifafanua kuwa ni vizuri kutoa kipaumbele kwa mashauri yanayohusisha makundi hayo yenye changamoto kwa kuhakikisha yanamalizika ndani kwa kipindi cha miezi sita tangu yalipofunguliwa, ikiwemo kuweka mazingira rafiki wakati wanapofika  mahakamani

Aidha alisema ni vema kutumia wataalamu lugha za ishara kwa mashahidi ya watu wenye ulemavu wa kutosikia au kuongea, kuhakikisha wanapata mwenendo, tuzo na amri za mbalimbali zinatolewa katika mashauri ya makundi hayo, kutoa nakala za hukumu kwa wakati, ikiwemo msaada wa kisheria pale inapobidi na kutumia kanuni tulizojifunza katika mashauri ya makundi yenye changamoto.

Aliwataka kujiongoza na kufanya yale waliyofundishwa uthabiti na pia ni sambamba  kwa kuzingatia miiko ya kazi wakiwa kama maafisa  mahakama ili kujenga imani kwa jamii. 

Alisema inapaswa kutambua mawasiliano yanayofanyika katika vyumba vya mahakama kwamba matendo yao yanaweza kuua au kuhuhisha, hivyo ni lazima kuwe na matendo ambayo yataweza kuhakikisha kwamba hisia zinalindwa na kutumia ufundi au namna mbalimbali ya kuhakikisha yale unayoweza kupata kwa shahidi anayetoka katika makundi hayo.

Aliushukuru uongozi wa Mahakama ya Tanzania, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Irish Rule of Law International (IRLI) kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo katika Kituo hicho.

Lengo   mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo mahakimu hao wa jinsi ya kuepuka kutonesha majeraha ya kisaikolojia kwa mashahidi na waathirika, hususani katika kesi za unyanyasaji wa kingono na ukatili wa kijinsia (Avoiding Re-traumatization) wanaposikiliza mashauri hayo.

 

Comments (0)

Leave a Comment