Post Details

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MHE. RAYMOND MWAIKASU AMEFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Raymond Mwaikasu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwake Tabata Segerea jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia ya Marehemu, mazishi ya Jaji Mstaafu Mwaikasu yatafanyika siku ya Jumanne Februari 23, 2021 nyumbani kwake Tabata Segerea.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 

Comments (0)

Leave a Comment