Post Details

HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO ILONGO-MBEYA AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Ilongo iliyopo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Mhe. Francis Mhagama kilichotokea Februari 13, 2021.

Mhe. Mhagama amefariki katika Hospitali ya Chimala alipokuwa akipatiwa matibabu.

Marehema Mhagama aliajiriwa na kujiunga na Mahakama Desemba 13, 2007. Alifanya kazi katika vituo mbalimbali vikiwemo vituo vya Lituhi wilayani Mbinga mkoani Ruvuma na Mahakama ya Mwanzo Ilongo wilayani Mbarali ambako alikuwa akifanya kazi mpaka wakati huu ambapo Mwenyezi Mungu alipoamua kumpumzisha.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.


                               BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 

Comments (0)

Leave a Comment