Post Details

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA MHE. REGINA RWEYEMAMU AMEFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Regina Rweyemamu aliyefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Kitengule iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam.

Kufuatia kifo hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salaam za rambirambi wa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Majaji, na watumishi wote wa Mahakama ya Tanzania.

"Nimepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa, natoa pole kwako na kwa Majaji wote na watumishi wa Mahakama, Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi", alisema Rais Magufuli.  

Msiba wa Jaji Mstaafu Rweyemamu uko nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

Taarifa Zaidi kuhusiana na msiba huu zitapatikana baadaye.

  BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments (0)

Leave a Comment