Post Details

MTENDAJI WA MAHAKAMA KANDA YA SHINYANGA AFARIKI DUNIA

Published By:Mary C. Gwera

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Shinyanga, Bw. Ignatio Kabale (pichani) kilichotokea alfajiri ya kuamkia leo Februari 12, 2021.

Taarifa za awali kutoka Kanda hiyo zinasema kuwa Marehemu Kabale alikutwa na umauti akiwa katika hospitali ya Serikali Bukoba mjini alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za mipango ya mazishi zitajulikana baadae.

Mahakama inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki cha majonzi cha kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 

Comments (0)

Leave a Comment