Post Details

HAKIMU MKAZI MFAWIDHI NANYUMBU AFARIKI DUNIA

Published By:Mary C. Gwera

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu-Mtwara, Marehemu Godfrey Mwambapa (pichani) kilichotokea leo Februari 11, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu zinasema kuwa marehemu alifikwa na umauti leo saa moja (1) asubuhi alipokuwa akipelekwa hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama Kanda ya Mtwara inasema kuwa ratiba ya kuaga mwili wa marehemu Mwambapa itafanyika Februari 12, 2021 kuanzia saa moja (01) asubuhi katika Hospitali ya Mkomaindo, Masasi.

Baada ya ratiba ya kuaga kukamilika, msafara kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili mazishi utaondoka kesho hiyohiyo kuanzia saa 02.30 asubuhi.

Mahakama inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao.

 BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

 

 

 

Comments (0)

Leave a Comment