Published By: | LYDIA CHURI |
---|
TANZIA
Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Mexsensius Lilundilu kilichotokea leo Januari 13 katika hospitali ya Kardinali Rugambwa iliyoko Ukonga Mombasa jijini Dar es salaam.
Taratibu nyingine za mazishi ya mtumishi huyo ambaye alikuwa ni Fundi Sanifu wa Mahakama Kuu ya Tanzania zitajulikana hapo baadaye.
Bwana Alitoa ana Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe