Post Details

MTUMISHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bi. Rose Wallace Msawa (Msaidizi wa Ofisi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga) aliyefariki dunia juzi Desemba 19, 2020 katika hospitali ya Bombo mkoani Tanga alipokuwa akipatiwa matibabu. 

Mwili wa Marehemu Rose Msawa umesafirishwa kwenda nyumbani kwao katika Kijiji cha Kilulu wilayani Muheza Mkoa wa Tanga kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Desemba 22, 2020.

Marehemu alizaliwa Novemba 23, mwaka 1963 ambapo baada ya kupata elimu aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania kama Msaidizi wa Ofisi na baadaye kupanda cheo na kufikia ngazi ya Msaidizi wa Ofisi Mkuu April 4, 2018.

     MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI

Comments (0)

Leave a Comment