Post Details

JAJI MKUU PROF JUMA AWAAPISHA MAHAKIMU WAKAZI WAPYA WAWILI

Published By:Mary C. Gwera

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma mapema leo Desemba 15, 2020 amewaapisha Mahakimu Wakazi wawili wa Mahakama za Mwanzo na kufanya idadi ya jumla ya Mahakimu wapya 41 waliopishwa leo na Novemba 27 mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mhe Jaji Mkuu amewaasa Mahakimu hao kufanya kazi kwa haraka ili kuendana na  kasi ya karne ya 21.

“Ninyi ni Mahakimu wa karne ya 21, hivyo ni muhimu kuendana na kasi ya karne hii kwa manufaa ya Mahakama na Taifa kwa ujumla,” alisema Mhe. Jaji Prof. Juma.

Aidha, Mhe. Jaji Mkuu aliwasisitiza Mahakimu hao kufanya kazi kwa kufuata viapo vyao kwa kutoa haki kwa wananchi bila upendeleo wa aina yoyote.

“Ninyi ndio sura ya Mahakama, hivyo ni vyema mkafanya kazi kwa kufuata maadili yaliyopo ili kutochafua taswira ya Mahakama,” alisisitiza Mhe. Jaji Mkuu.

Upatikanaji wa idadi hiyo ya Mahakimu utasaidia kuongeza nguvu kazi Mahakamani na hatimaye huduma ya utoaji haki kutolewa kwa wakati.

Comments (0)

Leave a Comment