Post Details

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA YA RUFANI MHE. NSEKELA AMEFARIKI

Published By:Mary C. Gwera

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Mhe. Harold Nsekela amefariki Dunia leo asubuhi, Desemba 06, 2020 mjini Dodoma baada ya kuugua kwa muda Mfupi.

Taarifa Zaidi kufuatia Msiba huo pamoja na taratibu nyingine za mazishi zitajulikana baadaye.

Marehemu Jaji Mstaafu Nsekela alizaliwa Oktoba 21 mwaka 1944.

Wadhifa wa Jaji

Marehemu Jaji Harold Nsekela aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na mwezi Februari mwaka 2003 marehemu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, nafasi aliyoitumikia mpaka alipostaafu kwa mujibu wa Sheria.

Marehemu Jaji Harold Nsekela aliteuliwa kuwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mwezi Desemba, 2016, wadhifa aliokuwa nao mpaka alipofariki leo asubuhi.

Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe

 

Comments (0)

Leave a Comment