Post Details

MTUMISHI WA MAHAKAMA YA MWANZO IKWIRIRI-RUFIJI AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI


Uongozi wa Mahakama ya Tanzania unasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bwn. Jumanne Omar Mbonde aliyekuwa Mlinzi Mwandamizi wa Mahakama ya Mwanzo Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.

Bwn. Mbonde alifariki Dunia jana tarehe 19/11/2020 katika kituo cha Afya Ikwiriri alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa shinikizo la Damu.

 Mwili wa Marehemu Mbonde umezikwa leo Rufiji mkoani Pwani.

Marehemu Jumanne Mbonde alizaliwa Aprili 20 mwaka 1968 wilayani Rufiji na baadaye aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania Oktoba 1 mwaka 2004 kama Mlinzi. Hadi mauti inamfika, Marehemu alikuwa ni Mlinzi Mwandamizi.

                                                            Inna Lillah wa Inna layhi Rajiun.

Comments (0)

Leave a Comment