Post Details

ELIMU YA UENDESHAJI MASHAURI YA UCHAGUZI ITUMIKE KULETA TIJA; JAJI BENHAJJ

Published By:Mary C. Gwera

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Benhajj Shaaban Masoud amewataka Wasaidizi wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani kutumia vyema elimu ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi ili kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya sheria na haki nchini.

Akifunga rasmi Mafunzo hayo Oktoba 16 mwaka huu yaliyofanyika kwa siku tatu katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji Dkt Masoud aliwaeleza washiriki kwamba, imani ya wananchi ni kuwa, Mahakama ni mahali pa kupata haki, hivyo basi Maafisa wa Mahakama wanatakiwa kutambua muhimu walionao kwa wananchi wanaowahudumia.

 “Ninawasihi sana kujiepusha na rushwa, kataeni rushwa, kemeeni rushwa na toeni elimu pale mnapopata nafasi na uwezo wa kufanya hivyo juu ya madhara ya rushwa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi”

Aidha, aliendelea kwa kuwaomba Maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kutekeleza majukumu anayopewa Jaji husika kwa wakati na pia kwa viwango bora.

Kwa upande mwingine, Mhe. Dkt Masoud aliwapongeza wawezeshaji wa mafunzo kwa jinsi walivyoendesha mafunzo hayo kwa umahiri mkubwa.

Comments (0)

Leave a Comment