Post Details

HAKIMU WA MAHAKAMA YA WILAYA YA CHUNYA AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

                                                                                   TANZIA

HAKIMU WA` MAHAKAMA YA MWANZO CHUNYA WILAYANI MBEYA MHE. ZAKOLEO LAMECK SANGA AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA

TAREHE 7/10/2020 KATIKA MJI MDOGO WA MAFINGA MKOANI IRINGA BAADA YA KUPATA AJALI YA GARI.

MWILI WA MAREHEMU ULISAFIRISHWA USIKU WA KUAMKIA JANA TAREHE 8/10/2020 KUREJESHWA NYUMBANI KWAO ENEO LA IWAMBI/TAZARA

MAZIWA, JIJINI MBEYA AMBAPO ULIAGWA JANA KABLA YA KUSAFIRISHWA KWENDA UWANJI WILAYANI MAKETE MKOANI NJOMBE KWA MAZISHI.

MAREHEMU ALIAJIRIWA KAMA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO NA KUFANYA KAZI KATIKA KITUO CHA MAHAKAMA YA MWANZO

CHUNYA MJINI KUANZIA DESEMBA, 2007 MPAKA MAUTI YALIPOMKUTA.

AIDHA, KABLA YA KUWA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO, MAREHEMU ALIWAHI KUFANYA KAZI MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA

KITUO CHA MAHAKAMA KUU MASJALA YA MBEYA KAMA KARANI MSAIDIZI DARAJA LA I, CHEO ALICHOKITUMIKIA MPAKA DESEMBA 2007 ALIPOBADILI KADA NA KUWA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO.

MAREHEMU AMEACHA MKE NA WATOTO WATATU.

                                            BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments (0)

Leave a Comment