Post Details

TANZIA

Published By:LYDIA CHURI

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni Mhe. Rukia Juma Katembo amefariki Dunia leo Septemba 15, 2020 katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa Marehemu utazikwa leo saa 10:00 jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Dua ya kumuombea ilimefanyika saa 4:00 Asubuhi, nyumbani kwake Pugu Dampo Dar es salaam.

Marehemu Rukia Juma Katembo alizaliwa Desemba 1 mwaka 1962. Aliajiriwa na Mahakama ya Tanzania Julai 1 mwaka 1983. Vituo vya kazi alivyowahi kufanyia kazi ni pamoja na Kigamboni, Temeke, Buguruni, Ilala, Pangani, Magomeni, na Kinondoni ambapo ndiyo kituo chake cha mwisho cha kazi.

Marehemu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya Nyonga na alikuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbali zikiwemo Muhimbili na Ocean Road hadi alipofariki.

 

 

Comments (0)

Leave a Comment