Post Details

MAHAKAMA YA TANZANIA, CHUO KIKUU CAPE TOWN KUSHIRIKIANA KUBORESHA MFUMO WA KUTUNZA MAAMUZI

Published By:kansha.innocent

Na. Innocent Kansha-Mahakama

Mahakama ya Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika ya Kusini wenye lengo kuendeleza juhudi za kuboresha mfumo maalumu wa kutunza maamuzi ya kimahakama TanzLII na kutengeneza namna bora ya ufikiaji na upatikanaji bure wa Maamuzi, Sheria na Kanuni za Tanzania kwa njia ya Mtandao “TanzLII - Access Court Decisions and Laws of Tanzania for Free”.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo tarehe 29 Mei, 2023 Mahakama Kuu Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke jijini Dar es salaam kati ya Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Martin Chuma kwa upande wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva. Huku utiwaji saini huo ukishudiwa na  Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika.

Tukio hilo lilienda sambamba uzinduzi wa Tovuti ya TanzLII iliyofanyiwa uboreshaji mkubwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika.

Comments (0)

Leave a Comment