Post Details

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI LINDI YAANZA KUTUMIA MFUMO WA KURATIBU MALALAMIKO

Published By:magreth.kinabo

Na Hillary Lorry, Lindi

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Mhe. Consolata Singano amewataka watumishil wa Mahakama hiyo na Mahakama ya Wilaya ya Lindi kuwa makini kuhusu mada ya Mfumo wa Kuratibu Malalamiko ( Sema na Mahakama).

Mhe. Singano alitoa kauli hiyo, wakati wa alipofungua mafunzo ya mfumo huo, yaliyofanyika kwa siku moja katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi. 

Mafunzo hayo yalitolewa na Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Kanda ya Mtwara, Bw. Richard Matasha alisema mfumo huo ni sehemu ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa mwaka 2020-2025 unaoitaka Mahakama ya Tanzania kuhama kutoka kwenye matumizi makubwa ya karatasi kwenda kwenye Mahakama Mtandao.

“Dhumuni la kuanzishwa kwa mfumo huu wa kuratibu malalamiko siyo kupokea malalamiko tu bali ni kutoa mrejesho kuhusu malalamiko yaliyopokelewa, kupata maoni,pongezi na mapendekezo  kutoka kwa wateja wa nje ambao ni wananchi na wateja wa ndani ambao ni watumishi juu ya huduma zinazotolewa na Mahakama ya Tanzania ” alisema Matasha.

Matasha aliongeza kuwa mfumo huo  utarahisisha  upokeaji wa malalamiko mengi kwa wakati moja, kuboresha utendaji wa kazi, utatuzi wa malalamiko na upatikanaji takwimu sahihi za malalamiko kwa wakati. Mfumo huo pia unategemewa kurejesha imani ya wananchi kwa Mahakama kwani mlalamikaji ataweza  kufuatilia lalamiko lake nakujua hatua iliyofikia  hata kwa njia ya simu ya kitochi maarufu kama “Kiswaswadu” popote alipo.

Kwa upande wa watumishi hao,walishukuru kwa kupatiwa mafunzo hayo na kuahidi kuongeza juhudi katika kuchapa kazi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.

 

Comments (0)

Leave a Comment

https://virtualclinic.mobi/