Post Details

MWILI WA JAJI BONGOLE WAZIKWA KIJIJINI KWAO ROMBO

Published By:LYDIA CHURI

Na Innocent Kansha -Mahakama, Rombo

Mwili wa aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Benedict Bongole umezikwa leo mchana katika  kijiji cha Shimbi Kati wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi ameongoza Waheshimiwa Majaji pamoja na Watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania katika mazishi hayo.

Marehemu Jaji Salvatory Bongole alifariki dunia Jumatano usiku, Julai 15, 2020 baada ya kuugua ghafla nyumbani kwake. Mwili wake ulisafirishwa siku ya Jumamosi Julai 18 baada ya Misa iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ikulu, Cheyo A mkoani Tabora.

 BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Comments (0)

Leave a Comment