Post Details

JAJI MFAWIDHI KANDA YA TABORA-SALVATORY BONGOLE AFARIKI DUNIA

Published By:LYDIA CHURI

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma anasikitika kutangaza kifo cha Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Bongole aliyefariki Dunia jana saa 5 usiku wa kuamkia leo baada ya Kuugua ghafla.

Jaji Bongole alipofikishwa hospitali ya Mkoa ya Kitete kwa matibabu, Daktari alithibitisha kuwa amefariki.

Taarifa Kuhusu Mipango ya Mazishi zitajulikana hapo baadaye.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE

Comments (0)

Leave a Comment